Zaburi 41:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Husema: “Maradhi haya yatamuua;hatatoka tena kitandani mwake!”

9. Hata rafiki yangu wa moyoni niliyemwamini,rafiki ambaye alishiriki chakula changu,amegeuka kunishambulia!

10. Ee Mwenyezi-Mungu, unionee huruma!Unipe nafuu, nami nitawalipiza.

11. Hivyo nitajua kwamba unapendezwa nami,maadui zangu wasipopata fahari juu yangu.

12. Wewe umenitegemeza kwani natenda mema;waniweka mbele yako milele.

13. Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli,tangu milele na hata milele!Amina! Amina!

Zaburi 41