2. Aliniondoa katika shimo la hatari,alinitoa katika matope ya dimbwi,akanisimamisha salama juu ya mwamba,na kuziimarisha hatua zangu.
3. Alinifundisha wimbo mpya,wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.Wengi wataona na kuogopa,na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.
4. Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu;mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno,watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo.
5. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umetufanyia mengi ya ajabu,na mipango yako juu yetu haihesabiki;hakuna yeyote aliye kama wewe.Kama ningeweza kusimulia hayo yote,idadi yake ingenishinda.
6. Wewe hutaki tambiko wala sadaka,tambiko za kuteketeza wala za kuondoa dhambi;lakini umenipa masikio nikusikie.
7. Ndipo niliposema: “Niko tayari;ninayotakiwa kufanya yameandikwa katika kitabu cha sheria;