Zaburi 35:5-14 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6. Njia yao iwe ya giza na utelezi,wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7. Maana walinitegea mitego bila sababu;walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8. Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,wanaswe katika mtego wao wenyewe,watumbukie humo na kuangamia!

9. Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10. Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.”

11. Mashahidi wakorofi wanajitokeza;wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12. Wananilipa mema yangu kwa mabaya;nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13. Lakini wao walipokuwa wagonjwa,mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;nilijitesa kwa kujinyima chakula.Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14. kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

Zaburi 35