25. Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”
26. Waache hao wanaofurahia maafa yangu,washindwe wote na kufedheheka.Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,waone haya na kuaibika.
27. Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia,wapaaze sauti kwa furaha waseme daima:“Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno!Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”