Zaburi 34:10-16 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa;lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema.

11. Njoni enyi vijana mkanisikilize,nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu.

12. Je, watamani kufurahia maisha,kuishi maisha marefu na kufurahia mema?

13. Basi, acha kusema mabaya,na kuepa kusema uongo.

14. Jiepushe na uovu, utende mema;utafute amani na kuizingatia.

15. Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu,na kusikiliza malalamiko yao;

16. lakini huwapinga watu watendao maovu,awafutilie mbali kutoka duniani.

Zaburi 34