Zaburi 33:13-22 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Mwenyezi-Mungu huangalia chini kutoka mbinguni,na kuwaona wanadamu wote.

14. Kutoka kwenye kiti chake cha enzi,huwaangalia wakazi wote wa dunia.

15. Yeye huunda mioyo ya watu wote,yeye ajua kila kitu wanachofanya.

16. Mfalme hawezi kuokolewa kwa kuwa na jeshi kubwa;wala shujaa hapati ushindi kwa nguvu zake kubwa.

17. Farasi wa vita hafai kitu kwa kupata ushindi;nguvu zake nyingi haziwezi kumwokoa mtu.

18. Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao,watu ambao wanatumainia fadhili zake.

19. Yeye huwaokoa katika kifo,huwaweka hai wakati wa njaa.

20. Mioyo yetu yamtumainia Mwenyezi-Mungu.Yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

21. Naam twafurahi kwa sababu yake;tuna matumaini katika jina lake takatifu.

22. Fadhili zako zikae nasi, ee Mwenyezi-Mungu,kwani sisi tumekuwekea tumaini letu.

Zaburi 33