8. Wewe hukuniacha nitiwe mikononi mwa maadui zangu;umenisimamisha mahali pa usalama.
9. Unionee huruma, ee Mwenyezi-Mungu, niko taabuni;macho yangu yamechoka kwa huzuni,nimeishiwa nguvu mwilini na rohoni.
10. Maisha yangu yamekwisha kwa majonzi;naam, miaka yangu kwa kulalamika.Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika;hata mifupa yangu imekauka.
11. Nimekuwa dharau kwa maadui zangu wote;kioja kwa majirani zangu.Rafiki zangu waniona kuwa kitisho;wanionapo njiani hunikimbia.
12. Nimesahaulika kama mtu aliyekufa;nimekuwa kama chungu kilichovunjikavunjika.
13. Nasikia watu wakinongonezana,vitisho kila upande;wanakula njama dhidi yangu,wanafanya mipango ya kuniua.
14. Lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu.Nasema: “Wewe ni Mungu wangu!”
15. Maisha yangu yamo mikononi mwako;uniokoe na maadui zangu,niokoe na hao wanaonidhulumu.
16. Uniangalie kwa wema mimi mtumishi wako;uniokoe kwa fadhili zako.
17. Usiniache niaibike ee Mwenyezi-Mungu,maana mimi ninakuomba;lakini waache waovu waaibike,waache wapotelee kwa mshangao huko kuzimu.
18. Izibe midomo ya hao watu waongo,watu walio na kiburi na majivuno,ambao huwadharau watu waadilifu.
19. Jinsi gani ulivyo mwingi wema wako,uliowawekea wale wanaokucha!Wanaokimbilia usalama kwakowawapa mema binadamu wote wakiona.