Zaburi 30:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mimi nilipofanikiwa, nilisema:“Kamwe sitashindwa!”

7. Kwa wema wako, ee Mwenyezi-Mungu,umeniimarisha kama mlima mkubwa.Lakini ukajificha mbali nami,nami nikafadhaika.

8. Nilikulilia wewe, ee Mwenyezi-Mungu;naam niliomba dua kwako ee Mwenyezi-Mungu:

9. “Je, utapata faida gani nikifana kushuka hadi kwa wafu?Je, mavumbi ya wafu yanaweza kukusifu?Je, yanaweza kusimulia uaminifu wako?

10. Usikie, ee Mwenyezi-Mungu, unihurumie;ee Mwenyezi-Mungu, unisaidie!”

11. Wewe umegeuza maombolezo langu kuwa ngoma ya furaha;umeniondolea huzuni yangu, ukanizungushia furaha.

12. Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya.Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.

Zaburi 30