2. Waovu wakinishambulia,na kutaka kuniangamiza,hao wapinzani wangu watajikwaa na kuanguka.
3. Hata jeshi likinizunguka,moyo wangu hautaogopa kitu;hata nikikabiliwa na vita,bado nitakuwa na tumaini.
4. Jambo moja nimemwomba Mwenyezi-Mungu,nalo ndilo ninalolitafuta:Nikae nyumbani mwa Mwenyezi-Mungusiku zote za maisha yangu;niuone uzuri wake Mwenyezi-Mungu,na kutafuta maongozi yake hekaluni mwake.
5. Siku ya taabu atanificha bandani mwake;atanificha katika hema lake,na kunisalimisha juu ya mwamba.
6. Nami kwa fahari nitaangalia juuya maadui zangu wanaonizunguka.Nitamtolea tambiko kwa shangwe hekaluni mwake,nitaimba na kumshangilia Mwenyezi-Mungu.