8. Ee Mwenyezi-Mungu, napenda makao yako,mahali unapokaa utukufu wako.
9. Usiniangamize pamoja na wenye dhambi,wala usinitupe pamoja na wauaji,
10. watu ambao matendo yao ni maovu daima,watu ambao wamejaa rushwa.
11. Lakini mimi ninaishi kwa unyofu;unihurumie na kunikomboa.
12. Mimi nimesimama mahali palipo imara;nitamsifu Mwenyezi-Mungu katika kusanyiko kubwa.