Zaburi 26:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, unitetee,maana nimeishi bila hatia,nimekutumainia wewe bila kusita.

2. Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima;uchunguze moyo wangu na akili zangu.

3. Fadhili zako ziko mbele ya macho yangu,ninaishi kutokana na uaminifu wako.

4. Sijumuiki na watu wapotovu;sishirikiani na watu wanafiki.

5. Nachukia mikutano ya wabaya;wala sitajumuika na waovu.

Zaburi 26