1. Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?Mbona uko mbali sana kunisaidia,mbali na maneno ya kilio changu?
2. Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu;napiga yowe usiku, lakini nafuu sipati.
3. Hata hivyo, wewe ni mtakatifu;wewe watawala na kusifiwa na Waisraeli.
4. Wazee wetu walikutegemea;walikutegemea, nawe ukawaokoa.
5. Walikulilia wewe, wakaokolewa;walikutegemea, nao hawakuaibika.
6. Lakini mimi ni mdudu tu, wala si mtu;nimepuuzwa na kudharauliwa na watu.
7. Wote wanionao hunidhihaki;hunifyonya na kutikisa vichwa vyao.
8. Husema: “Alimtegemea Mwenyezi-Mungu,basi, Mungu na amkomboe!Kama Mungu anapendezwa naye,basi, na amwokoe!”