Zaburi 20:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua,atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni;kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.

7. Wengine hujigamba kwa magari ya vita;wengine hujigamba kwa farasi wao.Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

8. Hao watajikwaa na kuanguka;lakini sisi tutainuka na kusimama imara.

9. Umjalie mfalme ushindi, ee Mwenyezi-Mungu;utujibu wakati tunapokuomba.

Zaburi 20