4. Akujalie unayotamani moyoni mwako,aifanikishe mipango yako yote.
5. Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako;tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu.Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!
6. Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua,atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni;kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.
7. Wengine hujigamba kwa magari ya vita;wengine hujigamba kwa farasi wao.Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
8. Hao watajikwaa na kuanguka;lakini sisi tutainuka na kusimama imara.