Zaburi 18:39-46 Biblia Habari Njema (BHN)

39. Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;uliwaporomosha maadui chini yangu.

40. Uliwafanya maadui zangu wakimbie,na wale walionichukia niliwaangamiza.

41. Walipiga yowe lakini hapakuwa na wa kuwaokoa;walimlilia Mwenyezi-Mungu lakini hakuwajibu.

42. Niliwatwanga wakawa kama vumbi inayopeperushwa na upepo;niliwakanyaga kama tope la njiani.

43. Wewe uliniokoa na mashambulizi ya watu,ukanifanya mtawala wa mataifa.Watu nisiowajua walinitumikia.

44. Mara waliposikia habari zangu walinitii.Wageni walinijia wakinyenyekea.

45. Wageni walikufa moyo;wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka.

46. Mwenyezi-Mungu yu hai!Asifiwe mwamba wa usalama wangu;atukuzwe Mungu wa wokovu wangu.

Zaburi 18