Zaburi 18:37-42 Biblia Habari Njema (BHN)

37. Niliwafuatia adui zangu na kuwakamata;sikurudi nyuma mpaka nimewaangamiza.

38. Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena;walianguka chini ya miguu yangu.

39. Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;uliwaporomosha maadui chini yangu.

40. Uliwafanya maadui zangu wakimbie,na wale walionichukia niliwaangamiza.

41. Walipiga yowe lakini hapakuwa na wa kuwaokoa;walimlilia Mwenyezi-Mungu lakini hakuwajibu.

42. Niliwatwanga wakawa kama vumbi inayopeperushwa na upepo;niliwakanyaga kama tope la njiani.

Zaburi 18