Zaburi 17:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu,uniokoe mikononi mwa watu hao,watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. Uwajaze adhabu uliyowawekea,wapate ya kuwatosha na watoto wao,wawaachie hata na wajukuu zao.

15. Lakini mimi nitauona uso wako, kwani ni mwadilifu;niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona.

Zaburi 17