1. Unilinde ee Mungu;maana kwako nakimbilia usalama.
2. Namwambia Mungu: “Wewe u Bwana wangu;sina jema lolote ila wewe.”
3. Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini,kukaa nao ndiyo furaha yangu.
4. Lakini wanaoabudu miungu mingine,watapata mateso mengi.Tambiko ya damu sitaitolea kamwe,na majina ya miungu hiyo sitayataja.