Zaburi 12:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Fanya haraka, ee Mwenyezi-Mungu!Watu wema wamekwisha;waaminifu wametoweka miongoni mwa watu.

2. Kila mmoja humdanganya mwenzake,husema kwa kudanganya na kwa moyo wa unafiki.

3. Ee Mwenyezi-Munguuikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu,na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia.

4. Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo tunayo, nani awezaye kututawala?”

5. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Kwa sababu maskini wanadhulumiwa,na wahitaji wanapiga kite, sasa naja,nami nitawapa usalama wanaoutazamia.”

Zaburi 12