Yoshua 19:17-23 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Kura ya nne ilizipata koo za kabila la Isakari.

18. Eneo lenyewe lilikuwa na miji ya Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,

19. Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,

20. Rabithi, Kishioni, Ebesi,

21. Remethi, En-ganimu, En-hada na Beth-pasesi.

22. Kadhalika, mpaka wao ulifika Tabori, Shahasuma, Beth-shemeshi na kuishia kwenye mto Yordani. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake.

23. Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Isakari; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19