31. nusu ya Gileadi, Ashtarothi, Edrei, ambayo ilikuwa chini ya himaya ya mfalme Ogu wa Bashani; Eneo hili walipewa nusu ya wazawa wa Makiri mwana wa Manase, kulingana na koo zao.
32. Mose alikuwa amewagawia sehemu hizo mbalimbali za nchi iliyokuwa mashariki ya Yeriko na Yordani, wakati alipokuwa kwenye tambarare za Moabu.
33. Lakini kabila la Lawi, Mose hakulipa sehemu yao ya nchi, maana aliwaambia kwamba sehemu yao itakuwa kumhudumia Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.