10. Kisha Yoshua akawaamuru viongozi wa watu,
11. “Piteni katika kambi na kuwaamrisha watu watayarishe chakula, kwa kuwa baada ya siku tatu mtavuka mto Yordani, kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapeni iwe mali yenu.”
12. Yoshua akawaambia watu wa kabila la Reubeni na Gadi na nusu ya kabila la Manase: