Yohane 6:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)

6. (Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.)

7. Filipo akamjibu, “Mikate ya fedha dinari 200 haiwatoshi watu hawa hata kama kila mmoja atapata kipande kidogo tu!”

8. Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,

9. “Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”

Yohane 6