Yohane 20:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani.

6. Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda,

7. na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.

8. Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyetangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaamini. (

9. Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka kwa wafu).

10. Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani.

Yohane 20