5. Yesu aliwapenda Martha, dada yake na Lazaro.
6. Alipopata habari kwamba Lazaro ni mgonjwa, Yesu aliendelea kukaa mahali hapo alipokuwa kwa siku mbili zaidi.
7. Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni tena Yudea!”
8. Wanafunzi wakamwambia, “Mwalimu! Muda mfupi tu umepita tangu Wayahudi walipotaka kukuua kwa mawe, nawe unataka kwenda huko tena?”