Yobu 40:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Nilithubutu kusema na sitasema tena.Nilisisitiza lakini sitaendelea kusema zaidi.”

6. Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga:

7. “Jikaze kama mwanamume.Nitakuuliza, nawe utanijibu.

8. Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu,kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia?

9. Je, una nguvu kama mimi Mungu?Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu?

10. “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu,ujipambe kwa utukufu na fahari.

11. Wamwagie watu hasira yako kuu;mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha.

12. Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha,uwakanyage waovu mahali walipo.

Yobu 40