Yobu 40:23-32 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Mto ukifurika haliogopi,halitishiki hata mto Yordani ukilifurikia kinywani.

24. Nani awezaye kuliziba macho na kuliteka?Nani awezaye kulitoboa pua kwa mtego?

25. Je, waweza kuvua dude Lewiyathani kwa ndoana,au kuufunga ulimi wake kwa kamba?

26. Je, unaweza kulitia kamba puani mwake,au kulitoboa taya kwa kulabu?

27. Je, wadhani litakusihi uliachilie?Je, litazungumza nawe kwa upole?

28. Je, litafanya mapatano nawe,ulichukue kuwa mtumishi wako milele?

29. Je, utacheza nalo kama ndege,au kulifunga kamba licheze na wajakazi wako?

30. Wadhani wavuvi watashindania bei yake?Je, wafanyabiashara watathubutu kulikata na kugawana?

31. Je, waweza kuichoma ngozi yake kwa mikuki,au kichwa chake kwa mfumo wa kuvua samaki?

32. Jaribu tu kuligusa, uone cha mtema kuni;Kamwe hutarudia tena kufanya hivyo!

Yobu 40