Yobu 4:16-21 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Kitu kilisimama tuli mbele yangu,nilipokitazama sikukitambua kabisa.Kulikuwa na umbo fulani mbele yangu;kulikuwa kimya, kisha nikasikia sauti.

17. Binadamu afaye aweza kuwa mwadilifu mbele ya Mungu?Mtu aweza kuwa safi mbele ya Muumba wake?

18. Hata watumishi wake, Mungu hana imani nao;na malaika wake huwaona wana kosa;

19. sembuse binadamu viumbe vya udongo,watu ambao chanzo chao ni mavumbi,ambao waweza kupondwapondwa kama nondo!

20. Binadamu kwa masaa machache tu waweza kuangamia;huangamia milele bila kuacha hata alama yao!

21. Iwapo uzi unaoshikilia uhai wao ukikatwawao hufa tena bila kuwa na hekima.

Yobu 4