19. “Je, Yobu, ndiwe uliyewapa farasi nguvu,ukawavika shingoni manyoya marefu?
20. Je, ni wewe unayemfanya farasi aruke kama nzige?Mlio wake wa maringo ni wa ajabu!
21. Huparapara ardhi mabondeni kwa pupa;hukimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote.
22. Farasi huicheka hofu, na hatishiki;wala upanga hauwezi kumrudisha nyuma.
23. Silaha wachukuazo wapandafarasi,hugongana kwa sauti na kungaa juani.
24. Farasi husonga mbele, akitetemeka kwa hasira;tarumbeta iliapo, yeye hasimami.
25. Kila ipigwapo tarumbeta, yeye hutoa sauti;huisikia harufu ya vita toka mbali,huusikia mshindo wa makamandawakitoa amri kwa makelele.
26. “Je, mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka,na kunyosha mabawa yake kuelekea kusini?