19. Huenda kulala tajiri, lakini ni mara ya mwisho;atafungua macho yake, na utajiri wake umetoweka!
20. Vitisho humvamia kama mafuriko;usiku hukumbwa na kimbunga.
21. Upepo wa mashariki humpeperusha akatoweka;humfagilia mbali kutoka makao yake.
22. Upepo huo humvamia bila huruma;atajaribu kuukimbia lakini mbio za bure.
23. Upepo humzomea akimbiapo,na kumfyonya toka mahali pake.