1. Yobu akaendelea kutoa hoja yake, akasema:
2. “Naapa kwa Mungu aliye hai,aliyeniondolea haki yangu,Mungu Mwenye Nguvu aliyeifanya nafsi yangu iwe na uchungu!
3. Naapa kuwa kadiri ninavyoweza kupumua,roho ya Mungu ikiwa bado ndani yangu;
4. midomo yangu kamwe haitatamka uongo,wala ulimi wangu kusema udanganyifu.
5. Siwezi kabisa kusema kuwa nyinyi mnasema ukwelimpaka kufa kwangu nasema sina hatia.
6. Nashikilia unyofu wangu, wala sitauacha;katika dhamiri yangu sina cha kunihukumu maishani mwangu.
7. “Adui yangu na apate adhabu ya mwovu,anayeinuka kunilaumu aadhibiwe kama mbaya.