Yobu 26:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Yobu akajibu:

2. “Aa! Jinsi gani ulivyomsaidia asiye na uwezo!Jinsi gani ulivyomwokoa asiye na nguvu!

3. Jinsi gani ulivyomshauri asiye na hekima,na kumshirikisha ujuzi wako!

4. Lakini umetamka hayo kwa ajili ya nani?Nani aliyekusukuma kuongea hivyo?”Bildadi akajibu:

5. “Mizimu huko chini yatetemeka,maji ya chini na wakazi wake yaogopa.

6. Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu.Abadoni haina kifuniko chochote.

Yobu 26