Yobu 23:5-11 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Ningeweza kujua atakachonijibu,na kuelewa atakachoniambia.

6. Je, angeshindana nami kwa nguvu zake zote?La! Bila shaka angenisikiliza.

7. Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu,Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele.

8. “Tazama, nakwenda mbele, lakini simpati,narudi nyuma, lakini siwezi kumwona.

9. Namtafuta upande wa kushoto lakini simwoni;nageukia kulia, lakini siwezi kumwona.

10. Lakini yeye anajua njia ninayofuata;atakapomaliza kunijaribunitatoka humo safi kama dhahabu.

11. Nafuata nyayo zake kwa uaminifunjia yake nimeishikilia wala sikupinda.

Yobu 23