18. Lakini Mungu ndiye aliyejaza nyumba zao fanaka,lakini walimweka mbali na mipango yao!
19. Wanyofu huona na kufurahi,wasio na hatia huwacheka na kuwadharau,
20. Wanasema ama kweli maadui zetu wameangamizwa,na walichobakiza kimeteketezwa kwa moto.
21. “Sasa, Yobu, kubaliana na Mungu uwe na amani,na hapo mema yatakujia.
22. Pokea mafundisho kutoka kwake;na yaweke maneno yake moyoni mwako.
23. Ukimrudia Mungu na kunyenyekea,ukiondoa uovu mbali na makao yako,