Yobu 20:25-29 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Mshale utachomolewa kutoka mwilini mwake;ncha yake itatolewa mgongoni mwake ikingaa,vitisho vya kifo vitamvamia.

26. Hazina zake zitaharibiwa,moto wa ajabu utamteketeza;kilichobaki nyumbani mwake kitateketezwa.

27. Mbingu zitaufichua uovu wake,dunia itajitokeza kumshutumu.

28. Mali zake zitanyakuliwakatika siku ya ghadhabu ya Mungu.

29. Hicho ndicho apewacho mtu mwovu kutoka kwa Mungu,ndicho mwovu alichopangiwa na Mungu.”

Yobu 20