23. Akiwa anajishughulisha kushibisha tumbo,Mungu atamletea ghadhabu yakeimtiririkie kama chakula chake.
24. Labda ataweza kuepa upanga wa chuma,kumbe atachomwa na upanga wa shaba.
25. Mshale utachomolewa kutoka mwilini mwake;ncha yake itatolewa mgongoni mwake ikingaa,vitisho vya kifo vitamvamia.
26. Hazina zake zitaharibiwa,moto wa ajabu utamteketeza;kilichobaki nyumbani mwake kitateketezwa.
27. Mbingu zitaufichua uovu wake,dunia itajitokeza kumshutumu.
28. Mali zake zitanyakuliwakatika siku ya ghadhabu ya Mungu.