Yobu 19:2-14 Biblia Habari Njema (BHN)

2. “Mtaendelea kunitesa mpaka lini,na kunivunjavunja kwa maneno?

3. Mara hizi zote kumi mmenishutumu.Je, hamwoni aibu kunitendea vibaya?

4. Hata kama ingekuwa nimekosa kweli,kosa langu lanihusu mimi mwenyewe.

5. Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza;mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu.

6. Jueni kwamba Mungu amenitendea vibaya,na kuninasa katika wavu wake.

7. Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’Lakini sijibiwi.Naita kwa sauti kubwa,lakini sipati haki yangu.

8. Njia yangu ameiziba kwa ukuta ili nisipiteamezitia giza njia zangu.

9. Amenivua fahari yangu;ameiondoa taji yangu kichwani.

10. Amenivunja pande zote, nami nimekwisha;tumaini langu amelingoa kama mti.

11. Ameichochea ghadhabu yake dhidi yangu;ameniona kuwa kama adui yake.

12. Majeshi yake yanijia kwa pamoja;yametengeneza njia ya kuja kwangu,yamepiga kambi kuizunguka nyumba yangu.

13. Mungu amewaweka ndugu zangu mbali nami;rafiki zangu wakuu wamenitoroka kabisa.

14. Jamaa zangu na marafiki hawanisaidii tena.

Yobu 19