Yobu 16:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Ningeweza kuwatia moyo kwa maneno yangu,na maneno yangu ya faraja yangewatuliza.

6. “Lakini nikisema maumivu yangu hayatulii,na nikikaa kimya hayaondoki.

7. Kweli Mungu amenichakazaameharibu kila kitu karibu nami.

8. Amenifanya ninyauke, na huo ni ushindi dhidi yangu.Kukonda kwangu kumenikabilina kushuhudia dhidi yangu.

9. Amenirarua kwa hasira na kunichukia;amenisagia meno;na adui yangu ananikodolea macho.

10. Watu wananidhihaki na kunicheka;makundi kwa makundi hunizunguka,na kunipiga makofi mashavuni.

Yobu 16