6. Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma,na udanganyifu juu ya udanganyifu.Wanakataa kunitambua mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
7. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema:Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu!Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu?
8. Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu,daima haziishi kudanganya;kila mmoja huongea vema na jirani yake,lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.
9. Je, nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya?Je, nisilipe kisasi kwa taifa kama hili?Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
10. Nitaililia na kuiomboleza milima;nitayaombolezea malisho nyikani,kwa sababu yamekauka kabisa,hakuna mtu apitaye mahali hapo.Hakusikiki tena sauti za ng'ombe;ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.
11. Mwenyezi-Mungu asema:“Nitaifanya Yerusalemu magofu matupu,naam, nitaifanya kuwa pango la mbweha;na miji ya Yuda nitaifanya kuwa jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu yeyote.”