4. Kila mmoja ajihadhari na jirani yake!Hata ndugu yeyote haaminiki,kila ndugu ni mdanganyifu,na kila jirani ni msengenyaji.
5. Kila mmoja humdanganya jirani yake,hakuna hata mmoja asemaye ukweli.Wamezifundisha ndimi zao kusema uongo;hutenda uovu kiasi cha kushindwa kabisa kutubu.
6. Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma,na udanganyifu juu ya udanganyifu.Wanakataa kunitambua mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
7. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema:Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu!Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu?