Yeremia 9:23-26 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mwenye hekima asijivunie nguvu zake,wala tajiri asijivunie utajiri wake.

24. Anayetaka kujivuna na ajivunie jambo hili:Kwamba ananifahamukwamba anajua Mwenyezi-Mungu hutenda mema,hufanya mambo ya haki na uadilifu duniani.Watu wa namna hiyo ndio wanipendezao.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

25. Mwenyezi-Mungu asema: “Siku zaja ambapo nitawaadhibu wote waliotahiriwa mwilini tu:

26. Wamisri, Wayuda, Waedomu, Waamoni, Wamoabu na wakazi wote wa jangwani wanaonyoa denge. Maana watu hawa wote na Waisraeli wote hawakutahiriwa moyoni.”

Yeremia 9