Yeremia 7:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu alimwamuru Yeremia aende kusimama

2. kwenye lango la hekalu lake Mwenyezi-Mungu na kutangaza ujumbe huu: “Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu enyi watu wa Yuda mnaoingia humu kumwabudu Mwenyezi-Mungu.

3. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Rekebisheni mienendo yenu na matendo yenu, nami nitawaacha mwendelee kukaa mahali hapa.

4. Msitumainie maneno haya ya uongo: ‘Hili ni hekalu la Mwenyezi-Mungu, hekalu la Mwenyezi-Mungu, naam hekalu la Mwenyezi-Mungu.’

5. “Ila kama mkibadili mienendo yenu na matendo yenu, mkitendeana haki kwa dhati;

Yeremia 7