Yeremia 6:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Hilo na liwe onyo kwako ee Yerusalemu,la sivyo nitakutupa kabisa kwa chuki;nikakufanya uwe jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu.”

9. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobakikama watu wakusanyavyo zabibu zote;kama afanyavyo mchumazabibu,pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”

10. Nitaongea na nani nipate kumwonya,ili wapate kunisikia?Tazama, masikio yao yameziba,hawawezi kusikia ujumbe wako.Kwao neno lako, ee Mwenyezi-Mungu,limekuwa jambo la dhihaka,hawalifurahii hata kidogo.

11. Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao.Nashindwa kuizuia ndani yangu.Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Imwage hasira barabarani juu ya watotona pia juu ya makundi ya vijana;wote, mume na mke watachukuliwa,kadhalika na wazee na wakongwe.

12. Nyumba zao zitapewa watu wengine,kadhalika na mashamba yao na wake zao;maana nitaunyosha mkono wangu,kuwaadhibu wakazi wa nchi hii.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

13. Wote, tangu mdogo hadi mkubwa kabisa,kila mmoja anatamani kupata faida isiyo halali.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja wao ni mdanganyifu.

Yeremia 6