Yeremia 51:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Babuloni ilikuwa kikombe cha dhahabumkononi mwa Mwenyezi-Mungu,ambacho kiliilewesha dunia nzima.Mataifa yalikunywa divai yake,hata yakapatwa wazimu.

8. Ghafla Babuloni imeanguka na kuvunjikavunjika;ombolezeni kwa ajili yake!Leteni dawa kutuliza maumivu yake;labda utaweza kuponywa.

9. Tulijaribu kuuponya Babuloni,lakini hauwezi kuponywa.Uacheni, twendeni zetu,kila mmoja katika nchi yake,maana hukumu yake ni kuu mnoimeinuka mpaka mawinguni.

10. Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia.Twendeni Siyoni tukatangazematendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

11. Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.Noeni mishale yenu!Chukueni ngao!

12. Twekeni bendera ya vitakushambulia kuta za Babuloni.Imarisheni ulinzi;wekeni walinzi;tayarisheni mashambulizi.Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekelezamambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.

13. Nchi hiyo imejaa mito na hazina tele,lakini mwisho wake umefika,uzi wa uhai wake umekatwa.

14. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake:“Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige,nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”

Yeremia 51