45. “Tokeni humo enyi watu wangu!Kila mtu na ayasalimishe maisha yake,kutoka hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
46. Msife moyo wala msiwe na hofu,kwa sababu ya uvumi mnaosikia nchini.Mwaka huu kuna uvumi huu,mwaka mwingine uvumi mwingine;uvumi wa ukatili katika nchi,mtawala mmoja dhidi ya mtawala mwingine.
47. Kweli siku zaja,nitakapoadhibu sanamu za Babuloni;nchi yake yote itatiwa aibu,watu wake wote watauawa humohumo.
48. Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomovitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni,waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
49. Babuloni umesababisha vifo duniani kote;sasa wenyewe utaangamizwa kwa mauaji ya Israeli.
50. “Nyinyi mlinusurika kifo,ondokeni sasa, wala msisitesite!Ingawa mko nchi ya mbali mkumbukeni Mwenyezi-Mungu,ukumbukeni pia mji wa Yerusalemu.
51. Mnasema: ‘Tumeaibishwa na kufadhaishwa;aibu imezifunika nyuso zetu,kwa sababu wageni wameingiakatika sehemu takatifu za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.’
52. “Kwa hiyo, wakati unakuja,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,ambapo nitaviadhibu vinyago vya Babuloni,na majeruhi watapiga kite katika nchi yake yote.
53. Ingawa Babuloni atapanda mpaka mbinguni,na kuziimarisha ngome zake ndefu,waangamizi watakuja kutoka kwangu kumvamia.2Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.