Yeremia 51:27-32 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Tweka bendera ya vita duniani,piga tarumbeta kati ya mataifa;yatayarishe mataifa kupigana naye;ziite falme kuishambulia;falme za Ararati, Mini na Ashkenazi.Weka majemadari dhidi yake;walete farasi kama makundi ya nzige.

28. Yatayarishe mataifa kupigana naye vita;watayarishe wafalme wa Medi, watawala na mawakili wao,tayarisheni nchi zote katika himaya yake.

29. Nchi inatetemeka na kugaagaa kwa maumivu,maana nia ya Mwenyezi-Mungu kuhusu Babuloni ni thabiti:Ataifanya nchi ya Babuloni kuwa jangwa,ataifanya iwe bila watu.

30. Askari wa Babuloni wameshindwa kupigana,wamebaki katika ngome zao;nguvu zao zimewaishia,wamekuwa kama wanawake.Nyumba za Babuloni zimechomwa moto,malango yake ya chuma yamevunjwa.

31. Tarishi baada ya tarishi wanapiga mbio,mjumbe mmoja anamfuata mjumbe mwingine,kumpasha habari mfalme wa Babulonikwamba mji wake umevamiwa kila upande.

32. Vivuko vya mto vimetekwa,ngome zimechomwa moto,askari wamekumbwa na hofu.

Yeremia 51