23. Ninakutumia kuponda wachungaji na makundi yao,wakulima na wanyama wao wa kulimia,wakuu wa mikoa na madiwani.
24. “Nitaiadhibu Babuloni na wakazi wote wa Kaldayo mkiona kwa macho yenu wenyewe, kwa sababu ya uovu wote walioufanya katika Siyoni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
25. Mimi ninapingana nawe ewe mlima mharibifu,mlima unaoharibu dunia nzima!Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.Nitanyosha mkono wangu dhidi yako,nitakuangusha kutoka miambani juuna kukufanya kuwa mlima uliochomwa moto;
26. hata hamna jiwe lako litakalochukuliwa kujengea,hakuna jiwe litakalochukuliwa kuwekea msingi!Utakuwa kama jangwa milele.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
27. Tweka bendera ya vita duniani,piga tarumbeta kati ya mataifa;yatayarishe mataifa kupigana naye;ziite falme kuishambulia;falme za Ararati, Mini na Ashkenazi.Weka majemadari dhidi yake;walete farasi kama makundi ya nzige.
28. Yatayarishe mataifa kupigana naye vita;watayarishe wafalme wa Medi, watawala na mawakili wao,tayarisheni nchi zote katika himaya yake.