9. Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya yote?Nisilipize kisasi juu ya taifa kama hili?
10. “Pandeni mpite katika mashamba yake ya mizabibumkaharibu kila kitu bila kumaliza kabisa.Yakateni matawi yake,kwani hayo si yangu mimi Mwenyezi-Mungu.
11. Naam, watu wa Israeli na watu wa Yuda,wamekosa kabisa uaminifu kwangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
12. Wamesema uongo juu ya Mwenyezi-Munguwamesema: “Hatafanya kitu;hatutapatwa na uovu wowote;hatutashambuliwa wala kuona njaa.
13. Manabii si kitu, ni upepo tu;maana neno lake Mungu halimo ndani yao.”Basi hayo na yawapate wao wenyewe!
14. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Kwa kuwa wao wamesema jambo hilo,sasa nitayafanya maneno niliyokupa wewe Yeremia kuwa moto.Watu hawa watakuwa kuni,na moto huo utawateketeza.
15. “Nami Mwenyezi-Mungu nasema juu yenu enyi Waisraeli:Mimi naleta taifa moja kutoka mbali,lije kuwashambulia.Taifa ambalo halishindiki,taifa ambalo ni la zamani,ambalo lugha yake hamuifahamu,wala hamwezi kuelewa wasemacho.