21. Sikilizeni enyi wajinga na wapumbavu;watu mlio na macho, lakini hamwoni,mlio na masikio, lakini hamsikii.
22. Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu!Kwa nini hamtetemeki mbele yangu?Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari,kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka.Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita;ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.
23. Lakini watu hawa wana moyo wa ukaidi na uasi;wameniacha wakaenda zao.
24. Wala hawasemi mioyoni mwao;‘Na tumche Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,anayetujalia mvua kwa wakati wake,anayetupatia mvua za masika na mvua za vuli;na kutupa majira maalumu ya mavuno.’
25. Makosa yenu yamewazuia msipate baraka hizo,dhambi zenu zimewafanya msipate mema.