8. Kimbieni enyi wakazi wa Dedani;geukeni mkaishi mafichoni!Maana nitawaleteeni maangamizienyi wazawa wa Esau;wakati wa kuwaadhibu umefika.
9. Wachuma zabibu watakapokuja kwenuhawatabakiza hata zabibu moja.Usiku ule wezi watakapofika,wataharibu kila kitu mpaka watosheke.
10. Lakini nimemnyanganya Esau kila kitu,naam, nimeyafunua maficho yake,wala hawezi kujificha tena.Watoto, ndugu na jirani zake wameangamizwa;hakuna hata mmoja aliyebaki.
11. Niachieni watoto wenu yatima nami nitawatunza;waacheni wajane wenu wanitegemee.”
12. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ikiwa wale ambao hawakustahili kunywa kikombe cha adhabu ni lazima wanywe, je, wewe utaachwa bila kuadhibiwa? La! Hutakosa kuadhibiwa; ni lazima unywe hicho kikombe!